Familia yalilia Haki baada ya mwanawao kuanguka ghorofani.
Familia moja kutoka Mikindani eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa inalilia haki baada ya mwana wao kuanguka kutoka ghorofa ya pili alipokuwa akiadhibiwa na kijakazi wa jirani.
Kulingana na waliyoshuhudia tukio hilo, mtoto huyo Kwa jina William Olando mwenye umri wa miaka 5 alikuwa amemfuata rafikiye anayeishi ghorofani humo kabla ya kupatikana na kijakazi aliyeanza kumuadhibu kwa kosa la kuingia katika nyumba hiyo bila ya idhini.
Mashahidi wa tukio Hilo wakiongozwa na Fatuma Ibrahim wamesema kuwa juhudi zao kumkataza kijakazi Huyo kutomuadhibu muathiriwa zilipuuzwa.
Aidha Fatuma amesema kuwa alikiripoti kisa hicho katika kituo cha pilisi cha Mikindani na tayari ameandikisha taarifa yake kuhusu tukio hilo.
Kwa upande wake Joseph Pepe ambaye ni Baba wa muathiriwa, anasema kuwa mwanawe amefanyiwa upasuaji kutokana na majeraha mabaya aliyoyapata katika sehemu tofauti za mwilini mwake ikiwemo figo.
Joseph hatahivyo ameonyesha kutoridhishwa na jinsi maafisa wa polisi wanavyoshughulikia kesi hiyo akiwataka kufanya uchunguzi kamili ili Haki itendeke Kwa mwanawe.
Hatahivyo akithibitisha tukio Hilo afisa mkuu wa polisi wa Eneo la Jomvu Peter Maluki amesema tayari polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo .