Mabaki wa miili wa waliongamia na ndege ya Ethiopina Airlines yawasili nchini.
Francis Mwaro
Mabaki ya miili ya wakenya ambao waliangamia katika ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines ya 302 imewasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi .
Mabaki ya miili hiyo imepokelewa na waziri wan chi za kigeni Monica Juma pamoja na waziri ya uchukuzi James Macharia
Idadi ya wakenya 36 ni miongoni mwa watu waliangamia katika mkasa huo ambao ulipoteza maisha ya watu 157.
Wawakilishi wa familia ambazo ziliathirika na mkasa huo waliandamana na mabaki ya wapendwa wao kutoka Addis Ababa nchini Ethiopia.
Idara ya kimataifa ya polisi imesema tiyari ilikuwa imemaliza shuguli ya kuitambua miili ya watu 157 ambao walikuwa wameabirindege hiyo ambayo ilikuwa imetoka Addis Ababa kuelekea jijini Nairobi.
Shirika la Interpol kupitia katibu wake Jurgen Stock lilimesema wataalamu 100 walihusika katika shuguli ya kuitambua miili hiyo na watu 48 walitambuliwa kupitia alama za vidole.
Hata hivyo shirika linalotengeneza ndege za Boeng lilitoa shilingi bilioni 5 ambao zitawalipa fidia familia ambazo ziliwapoteza wapendwa wao wakati wa mkasa huo kila familia ikiapata fidia ya shilingi milioni 15.