Vita dhidi ya bidhaa za magendo barabara kuu ya ukanda wa kaskazini vyachukuwa mkondo mpya

VITA  dhidi ya usafirishwaji wa bidhaa za magendo kupitia barabara ya ukanda wa kaskazini vimepata mwako mpya baada ya halmashauri ya kukabiliana na bidhaa za magendo nchini ACA kuingia katika mkataba wa maelewano na mamlaka ya kusimamia usafirishaji wa mizigo katika barabara kuu ya ukanda wa Kaskazini NCTTCA, unaonuia kukabiliana na tatizo hilo katika nchi wanachama .

Akizungumza katika kikao na wanahabari mjini Mombasa wakati wakutiwa sahihi kwa makubaliano hayo, Mwenyekiti wa bodi halmashauri ya ACA Josephat Kabeabea, amedokeza kuwa taifa la Kenya linapoteza mamilioni ya pesa kutokana na kusafirishwa kwa bidhaa za magendo kupitia barabara ya kaskazini, hivyo amesisistiza haja ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili katika juhudi za kukabilianana na usafirishwaji wa bidhaa ghushi humu nchini na mataifa wanachama wanaotumia barabara hiyo.

Kadhalika Mwenyekiti huyo amedokeza kuwa halmashauri ya ACA inajukumika kisheria kushirikiana na taasisi za kitaifa na za kimataifa katika jitihada za kukomesha usafaorishwaji wa bidhaa ghushi katika kanda hii.

Kwa upande wake katibu mkuu katika halmshauri ya kusimamia shughuli ya usafiri katika barabara kuu ya ukanda wa kaskazini NCTTCA Justus Omae ameupongeza ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili huku akisema kuwa kufuatia mkataba huo taasisi hizo sasa zitajukumika kikamilifu katika kitokomeza visa vya usafirishwaji wa bidhaa za magendo ambazo zimegharimu mataifa wananachama mabilioni ya pesa.

Hatahivyo mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya ACA daktari Robi Mbugua Njoroge amesema kuwa utekelezwaji wa mkataba huo utakuwa na changamoto kubwa endapo sheria za kukabiliana na bidhaa za magendo na biadhara haramu kati ya nchi wanachama hazitaoanishwa.

Utiwaji sahihi wa mkataba huo unajiri huku kukiripotiwa ongezeko la biashara haramu katika maeneo ya mipakani ambapo magenge ya wahalifu yamekuwa yakitumia barabara hiyo kusafairisha mizigo haramu .

https://ptirtika.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287