Maandamano ya kupinga sgr kuendelea kila siku ya Jumatatu.
Na Mosphine Mukodo
Vugu vugu la wafanyibiashara wa magari na madereva wa malori kwa mara nyengine hii leo wameandama tena wakiishinikiza serikali kusitisha mpango wa kusafirishamakasha ya mizigo kwa njia ya reli reli ya kisasa.
Vuguvugu hilo linalojiita OKOA MOMBASA likishirikiana na mashirika ya kutetea haki za binadamu la Haki Afrika na MUHURI linasema kamwe halitatishwa na viongozi wowote na wataendelea kufanya maandamamono kila siku ya Jumatatu hadi pale serikali itasitisha agizo hilo.
Mwenyekiti wa Vuguvugu hilo Salim Karama amewalaumu Viongozi wa eneo la Pwani kwa kushindwa kusimama kidete kuwatetea wakazi kufuatia athari ya utekelezwaji wa mpango huo.
Kwa upande wake Mshauri wa Masuala ya Kisheria katika Vuguvugu hilo Philip Jagero ameipa makataa ya masaa ishirini na nne Ofisi ya Mashtaka ya Umma kuwachukulia hatua za kisheria Mkuu wa Mamlaka ya Kodi, Mkuu wa Mamlaka ya Bandari ya Mombasa na Waziri Macharia kwa kutatiza biashara hiyo ambayo imekuwa ikitegemewa na wakazi wa Pwani.
Jagero pia amemulamu kiongozi wa cahama cha ODM Raila Odinga kwa kulinyamazia swala hilo akisema amelitenga eneo la pwani ambao muda wote limemuunga mkono wakati wa uchaguzi.
Vuguvugu hilo limesisitiza kwamba litaendelea na maandamano kila jumatatu ya kila wiki hadi pale kusitishwa kwa agizo hilo kutakapochapishwa rasmi kwenye gazeti la serikali.