Wakaazi wa Changamwe waonywa kutojenga nyumba kiholela

PHOTO: Courtesy

Wakaazi wa wadi ya Kipevu eneo bunge la Changamwe wametakiwa kuacha kujenga nyumba kiholela katika eneo hilo ili waweze kuepukana na mafuriko yanayoshuhudiwa kila mara mvua inaponyesha.

Mwakilishi wa wadi hiyo Faith Mwende Boniface amesema kuwa licha ya kufanya juhudi za kusafisha mitaro ya kupitishia maji taka kwa wakati muafaka bado tatizo hilo linashuhudiwa kutokana na njia za maji kuzibwa na baadhi ya majengo.

Hata hivyo mwakilishi huyo ametoa wito kwa wazazi kuwadhibiti watoto wao wakati wa mvua akisema chochote chaweza kutokea.

Aidha ameongeza kuwa ni wakati muafaka wa kushirikiana kwa kila jambo na kuacha lawama.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287