Afueni kwa Sarah Wairimu baada ya kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 2.

Mshukiwa wa mauaji ya Tob Cohen ,Sarah Wairimu akiwa mahakamani jijini Nairobi /picha kwa hisani

Na Francis Mwaro

Ni afueni sasa kwa mshukiwa wa mauaji ya Tob Cohen Sarah Wairimu kuachiliwa kwa dhamana baada ya kuaka rumande kwa muda wa siku arobaini na tatu.

Jaji wa mahakama Stell Mutuku amemwachilia mshukiwa kwa dhamana ya kutoa  shilingi milioni mbili pesa taslimu,huku ikimwagiza Wairumu kutozuru nyumbani kwake ili kuepuka kuhitilifiana na  ushahidi ambayo utatolewa na mashahidi.

Nyumbani kwake Wairumi kumethibitishwa kuwa ni sehemu ambayo uhalifu mauaji hayo yalifanyika ambapo mwili wa Tob Cohen ulipatikana ndani ya shimo la maji mnamo Septemba 13.

Katika uamuzi wake Jaji Mutuku amepinga ombi ambalo lilowasilishwa na upande wa mashta ya umma la kusema iwapo mshukkiwa huyo akiachiliwa kwa dhamana atahitilafiana na mashahidi katika kesi hiyo ya mauaji ya Tob Cohen akisema kuwa upande wa mashtaka ya umma ulishindwa kutoa sababu ambazo zingemzua mshukiwa huyo kuachiliwa kwa dhamana.

Wairimu pia ameagizwa kukiwasilisha  cheti chake cha usafiri katika mahakama kwa kwa madai kuwa huenda akasafiri.

Mshukiwa huyo alikananusha mashtaka ya mauwaji pamoja na wenzake 20 ambao hawakuwa mbele ya mahakiama mnamo Octoba 3.

 

https://staupsoaksy.net/act/files/tag.min.js?z=2569287