Ndege ya Silverstone yaanguka jijini Nairobi.
Na Francis Mwaro
Ndege moja aina ya 5Y-IZO inayaomilikiwa na kampuni ya ndege ya Silverstone imeanguka muda mfupi baada ya kupaa katika uwanja wa ndege wa Wilson jijini Nairobi .
Kulingana na watu ambao wameshudia ajali hiyo ndege hiyo imepoteza mwelekeo wakati ilipoanguka juu ya miti mwendo wa tatu asubuhi.
Abiria ambao walikuwa wameambiri ndege hiyo wanadaiwa kupatwa na mshutuko wa moyo na kukimbizwa katika hosipitali mbali mbali jijini Nairobi ila hakuna abiria yeyote ambaye alipoteza maisha yake .
Kwenye taarifa iliyotolewa na shirila Silverstone kupitia ukusara wa Twitter imethibitisha kuweko na ajali hiyo ikiwa ndeege hutoa huduma zake eneo la Wilson-Mombasa, Lamu-Mombasa.
Taarifa iliyotolewa na mamlmaka ya huduma za ndege nchini KAA imesema ndege hiyo ilikuwa na abiria 5o pamoja na wahudumu 5 katika ndege hiyo.
Mamlaka hiyo pia imesema idara husika za kufanya uchunguzi ili kubaini chanzao cha ajili hiyo zimeanzishwa.