Pombe haramu yanaswa na kuharibiwa kaunti ya Bomet
Maafisa wa polisi wamefanikiwa kunasa na kuharibu lita mia mbili ya pombe haramu aina ya changaa eneo la Cheptimtim kaunti ya Bomet.
Katika oparesheni hio iliyoendeshwa mapema hii leo maafisa hao pia wamefanikiwa kuwatia mbaroni washukiwa watano wa ugemaji na wauzaji pombe hio huku wakisubiri kufikishwa mahakamani hii leo.
Constabo spesheli wa polisi Alex Shikondi amedhibitisha hayo na kuwahakikishia wakaazi wa eneo hilo kuwa msako huo bado unaendelea .
Aidha afisa huyo amelalamika kwamba wanaoathirika na pombe hiyo ni watoto wao kwa hivyo amewahimiza wakaazi hao kushirikiana ili waweze kumaliza utumiaji na uzaji wa pombe haramu katika kaunti hiyo.