Maisha yangu yako hatarini- Mwakilishi wa wadi Likoni

PHOTO: Courtesy

Mwakilishi wa wadi ya Bofu huko Likoni kaunti ya Mombasa Ahmed Salama Omar, sasa anadai kwamba maisha yake yamo hatarini baada ya kuwekewa tuhuma ya ulanguzi wa dawa za kulevya siku chache zilizopita.

Akizungumza na wanahabari hapa Mombasa, Salama amesema shutma anazowekewa zinahusiana na msimamo wake wa kisiasa za uchaguzi mkuu wa 2022.

Salama amesema tangu madai hayo ya ulanguzi wa dawa za kulevya kuchipuka amekuwa akifuatiliwa na watu wasiojulikana na kumueka katika hali ya wasiwasi.

 

https://staupsoaksy.net/act/files/tag.min.js?z=2569287