Vihoja mahakamani Mombasa

By Munna Swaleh
Wanaume wawili wamefikishwa mahakamani mjini Mombasa na kushtakiwa makosa 8 ya kughushi stakabadhi ikiwemo ripoti ya dhamana (court bond valuation ).
Wawili hao Teddy Ojwang Mwanda na George Ochieng Omollo wamekabiliwa na mashtaka hayo hata hivyo wamekana mbele hakimu mkuu mkaazi Vincent Odet.
Wawili hao aidha walighushi stakabadhi hizo wakiwa na nia ya kusimamia mshukiwa mmoja dhamana.
Mahakama imeelezwa kuwa wawili hao walighushi stakabadhii ikiwemo KRA pin certificate, logbook ya gari na hata Kigali cha dhamana ya mahakama.
Wawili hao wameachiliwa kwa dhamana ya shillingi laki tano na mdhamini wa kiasi sawia na hicho au shillingi laki mbili pesa taslimu.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 16 mwezi huu.
Na katika mahakama hiyo hiyo…………………………………… Jasper Malava Ekesa ameshtakiwa na makosa 12 ikiwemo kosa la kughushi stakabadhi ili amsimamie mwenzake dhamana kwa jina Owen Mutuvi Joseph.
Mahakama imeelezwa kuwa mnamo tarehe 30 mwezi Agosti mwaka huu Ekesa walighushi barua ya kuonyesha ameajiriwa na serikali ya kaunti ya Mombasa, KRA pin ,barua za kuonyesha kuwa mwanachama wa Jitegemee Sacco, cheti cha mshahara na vyenginevyo.
Aidha pia alikabiliwa na shtaka la kutoa taarifa za uongo kwa hakimu mkaazi wa mahakama ya Shanzu David Odhiambo kuwa alikuwa mfanyikazi wa serikali ya kaunti ya Mombasa .
Hata hivyo amekana mashtaka yote na kuachiliwa kwa dhamana ya shillingi laki mbili na mdhamini wa kiasi sawia na hicho au shillingi laki moja pesa taslimu.
https://fenoofaussut.net/act/files/tag.min.js?z=2569287