Kundi la wanawake la Embrace Kenya lazuru Mombasa
Wanawake wa Kundi la Ebrace Kenya wamezuru uwanja wa Tononoka jijini Mombasa ambapo mkutano wao wa hadhara utafanyika kesho.
Wakiongozwa na Mbunge wa Likoni Mishi Mboko, akina mama hao wamekana madai kuwa mkutano wa kesho ni wa kisiasa wakisisitiza kwamba wanalenga kuhubiri amani.
Viongozi hao wamesema watazidi kuunga mkono ushirikiano baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Chama cha ODM Raila Odinga kwani umeleta utangamano nchini.