Odinga abisha hodi kwenye mradi wa Galana Kulalu kutathmini utendakazi wa mwanakandarasi
Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga anaratajiwa kuzuru mradi wa upanzi wa mahindi wa Galana Kulalu katika kaunti ya Kilifi leo hii.
Raila anatarajiwa kuangazia jinsi mradi huo wa shilingi bilioni 7.2 ulivyo kwa sasa baada ya kukumbwa na utata baada ya kampuni iliyopewa kandarasi hiyo ya nchini Israel kukumbwa na utata.
Kulingana na mhandishi wa bodi ya unyunyizadi maji ambao waliweza kuchukua mradi huo Raphael Ogendo , anasema kuwa mradi huo haujakwama kutokana na mwanakandarasi kujiondoa.
Ameongeza kuwa mradi huo uko na thamani kubwa sana ya pesa kwani unazalisha magunia mengi ya mahandi ambayo yanaleta faida.