Serikali ya kitaifa kuondoa karantini ya lazima kwa watalii
By Jeff Chiro
Serikali ya kitaifa imetakiwa kuondoa agizo la kuwekwa karantini ya lazima kwa watalii wanaozuru humu nchini kabla ya kuruhusiwa kuendelea na shughuli zao.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa muungano wa utalii Victor Shitaka ,hatua hiyo itazidi kulemaza sekta ya utalii ambayo inatarajiwa kurejea baada ya mipaka kufunguliwa vile vile usafiri wa angani kurejelea shuhuli zake.
Hata hivyo Shitaka ameishauri serikali kuwa watalii hao waruhusiwe kutumia vyeti vya vipimo vya virusi vya korona walivyopimwa wakitoka makwao.
Amesisitiza kuwa hoteli zote zinafanfa mikakati kuona kwamba msambao wa virusi vya korona unadhibitiwa.
Aidha amezitaka idara husika kuingilia kati kusitisha agizo hilo.