Usalama utadumishwa katika zoezi la censa- Rotich, Naibu Kamishna Kilifi
Naibu kamishena wa kaunti ya Kilifi eneo la Kaloleni Paul Rotich amesema polisi wamejipanga vilivyo kuhakikisha hakuna visa vya utovu wa usalama vinavyo shuhudiwa wakati wa zoezi la censa.
Akizungumza katika eneo la kaloleni, Rotich ametoawito kwa wakaazi wa eneo hilo kuhakikisha wamejitokeza kwa wingi kwa zoezi hilo akisema kuwa usalama utaimarishwa kila eneo.