Achoki ahamishwa kutoka kaunti ya Mombasa na kupelekwa Marsabit
Maafisa wa usalama 122 wa ngazi za chini kote nchini wamepokea uhamisho katika mageuzi yanayolenga kuboresha usalama nchini.
Hapa Mombasa kamishna wa polisi Evans Achoki amehamishwa hadi kaunti ya Marsabit hii ni baada ya waziri wa Maswala ya ndani Fred Matiangi kusema kwamba angefanya uhamisho huo kutokana na utovu wa usalama uliokithiri.
Vilevile, kamanda wa kaunti hiyo Jonstone Ipara amehamishwa hadi kaunti ya Uasin gishu kadhalika kamanda wa eneo la pwani Marcus Ochola kuhamishwa hadi eneo la bonde la ufa.
Hata hivyo Baadhi ya wakazi wameunga mkono kuhamishwa kwa maafisa wakuu wa usalama katika kaunti hiyo huku wengine wakitilia shaka ujio wa mafisa hao wapya wakisema kwamba huenda ikawachukua muda kufahamu mazingira halisi ya kaunti hiyo.