Mtu mmoja atiwa nguvuni baada ya kupatikana na pembe za ndovu

KENYA-IVORY-POACHING-POLICE

Raia mmoja wa uhispania ametiwa nguvuni na maafisa wa shirika la uhifadhi wa wanyama pori KWS katika uwanja wa kimataifa wa JKIA, akiwa na pembe ya ndovu ilio na uzito wa gramu ishirini na tano. Mshukiwa alikua akisafiri kutoka Nairobi kuelekea Dar es salaam Tanzania wakati aliponaswa .

Maafisa wa KWS wamesema kwamba, atawasilishwa mahakamani ambapo atashtakiwa kwa makosa ya ulanguzi . Mapema mwezi huu serikali ilizindua kampeni ya kusitisha biashara ya pembe za ndovu humu nchini. Kampeni hio inalenga kukabili biashara hio haramu hapa nchini na katika mataifa mbali mbali hapa duniani.

https://staupsoaksy.net/act/files/tag.min.js?z=2569287