Wakaazi walalamikia kupigwa na maafisa wa jeshi la majini

PHOTO: Courtesy

By Abubakar Ali

Wakazi wa eneo la Mtongwe kaunti ya Mombasa walalamikia kuhujumiwa na kupigwa na maafisa wa jeshi la majini.

Wakazi hao waliokuwa na majeraha baada ya kupigwa na kikosi hicho cha jeshi wamesema kuwa Kitendo hicho kimetokea baada ya kuuwawa kwa afisa wa jeshi.

Vile vile, afisa wa maswala ya dharura wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika Mathias shipetta, amesema kuwa wamesikitishwa na kitendo hicho kwani jukumu la maafisa wa jeshi kudumuisha usalama wala si kupiga wakazi wasio na hatia.

Aidha, ameitaka serikali Kuwachukulia hatua za kisheria maafisa hao.

 

 

 

 

https://fenoofaussut.net/act/files/tag.min.js?z=2569287