Vuta ni kuvute za Odinga na Ruto

PHOTO: Courtesy

Naibu wa Rais Daktar Willium Ruto ametangaza rasmi kuwa yuko tayari kushindana na Kinara wa ODM Raila Odinga katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.

Ruto aidha amemtaka Raila kuwaahidi wananchi kwamba iwapo atashindwa atakubali wamuzi wa wapiga kura na kuwepo nma amani baada ya mshindi kutangazwa na Tume ya uchaguzi IEBC.

Hata hivyo Odinga amepuzilia mbali taarifa zinazodai kwama ametangaza rasmi kuwa atawania kiti cha urais mwaka wa 2022.

Odinga ameeleza kusikitishwa na taarifa hiyo ambayo ilichapishwa wikendi na Gazeti moja la  Humu nchini likadai kwamba atakuwa miongoni mwa wale watakaowania kiti hicho na ndio sababu iliyosababisha kupatikana kwa mwafaka baina yake na Rais Uhuru Kenyatta almaarufu Handshake

Hayo yakijiri Mawakili wa Odinga wametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Gazeti lililochapisha habari kuashiria kwamba Odinga yuko katika kinyang’anyiro hicho cha mwaka 2022.

Hata hivyo Gazeti hilo limepewa saa 24 kurekebisha Taarifa hiyo.

 

 

 

 

https://fenoofaussut.net/act/files/tag.min.js?z=2569287