Spika wa bunge la kitaifa atangaza rasmi kiti cha kibera kuwa wazi
Huku zikiwa zimepita siku 17 tangu kufariki kwa mbunge wa Kibera Ken Okoth kutokana na saratani,Spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi amekitangaza rasmi kiti hicho kuwa wazi.
Wagombeaji mbali mbali wameonyesha hamu ya kuwania kiti hicho ambao ni aliyekuwa msaidizi wa kinara wa Chama cha ODM Eliud Owalo ,aliyekuwa Mbunge wa Embakasi Kusini Irshad Sumra, aliyekuwa Seneta Elizabeth Ongoro, Benson Musungu na Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna.
Baada ya wadhifa huo kutangazwa kuwa wazi, Tume ya Uchaguzi, IEBC inatarajiwa kuandaa uchaguzi mdogo chini ya kipindi cha miezi mitatu baada ya kupokea notisi rasmi kutoka kwa Muturi.