Husisheni polisi kusuluhisha mizozo ya malisho- Said Mwachenda, aliyekuwa diwani Mariakani

PHOTO: Courtesy

Siku chache tu baada ya mzee mmoja kuuliwa na wafugaji kutokana na mzozo wa malisho eneo la Mariakani, aliyekuwa diwani wa wodi ya Mariakani Said Mwachenda amesema kuwa sio vyema kwa wafugaji kulisha katika mashamba ya watu bila idhini kutoka kwa wahusika wa mashamba hayo.

Wakati huo huo ameitaka jamii kuhusisha vyombo vya usalama kila kunapotokea migogoro kama hiyo huku akivitaka vyombo hivyo kuchukua hatua ya haraka pindi kunapotokea shida ili kuona kuwa hakutokei maafa zaidi.

Hata hivyo ameitaka serikali kuja na mpango kuona kuwa hali kama hizo haziwakumbi wananchi na kutoa suluhu la haraka

https://staupsoaksy.net/act/files/tag.min.js?z=2569287