Rais Kenyatta atia saini mswada wa Takwimu
Rais Uhuru Kenyatta ametia saini kuwa sheria marekebisho ya mswaada wa Takwimu.Sheria inakusudiwa kulainisha usimazi wa takwimu katika serikali za kaunti pamoja na ile ya kitaifa kwa kuhakikisha kuwa ukusanyaji na utayarishaji wa takwimu unatekelezwa kulingana na desturi na viwango vya kimataifa.
Sheria hiyo mpya kuhusu takwimu pia inaimarisha jukumu la halmashauri ya kitaifa ya takwimu.