Wabunge waanze kutoa hoja zao bungeni kwa lugha ya kiswahili- Wadau
By Mohamed Mutakina
Wadau wa elimu wanazidi kushinikiza kutambuliwa kwa lugha ya Kiswahili na watoto kufunzwa kikamilifu katika shule zote ili kuweza kuiopa uhalisia wake miongoni mwa jamii.
Akizungumza na wanahabari naibu mwenyekiti wa chama cha KNUT tawi la Kilindini Ahmed Kombo amelitaka bunge la kitaifa kuanza kutoa hoja zake bungeni kwa lugha ya Kiswahili.
Kombo amesema kuwa endapo bunge litakuwa likitoa hoja zake Kiswahili basi litakuwa mfano wa kuigwa na wananchi wake.
Aidha amesema kuwa Kiswahili sasa kimetambulika kwingi akisema kwamba zaidi ya watu wapatao milioni mia mbili duniani huongea lugha ya Kiswahili.