Baba amlawiti mwanawe wa kiume, Mombasa

PHOTO: Courtesy

By Mohamed Ali

Mwanaume mmoja amemlawiti mwanawe wa kiume wa umri wa miaka 12 sehemu za Bakarani Kisauni katika kaunti ya Mombasa.

Mwanaume huyo anayedaiwa kuwa baba mzazi wa kijana huyo amesemekana kumtendea kitendo hicho kijana huyo, kila siku baada ya mamake mzazi kutoweka na kuwaacha wakiishi na baba huyo.

Vilevile, majirani waliomfumania mzee huyo akimlawiti kijana wake wamesema kuwa baba huyo amekumbwa na mashtaka sawia na hayo na hii si mara yake ya kwanza kutenda kitendo hicho kwani ameshtakiwa na kosa kama hilo mahakamani.

Kwa sasa majirani wanataka mzee huyo aweze kuchukuliwa hatua kali ili mtoto huyo apate haki.

https://pertawee.net/act/files/tag.min.js?z=2569287