Visa vya ugonjwa wa Ebola vyazidi kuripotiwa nchini Kongo

PHOTO: Courtesy

kisa cha pili cha ugonjwa wa Ebola kimebainika katika mji wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo unaopakana na Rwanda, kikiibua hofu ya kuwa ugonjwa huo unaoua unaweza kusambaa.

kisa hicho kilithibitishwa katika mji wa Goma, unaokaliwa na watu milioni mbili, maafisa wanasema.

Zaidi ya watu 1,600 wamekwisha kufa kutokana na Ebola katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo tangu mlipuko wa ugonjwa huo ulipotokea Agosti 2018.

Shirika la Afya duniani wiki iliyopita lilitangaza mlipuko wa ugonjwa huo kama dharura ya dunia ya afya.

Ni kiwango cha juu cha sauti ya dharura ambacho WHO linaweza kuitoa na imewahi kutolewa mara nne tu awali – ukiwemo mlipuko wa Ebola uliowakumba watu wa Afrika Magharibi kuanzia mwaka 2014 hadi 2016, ambao uliwauwa zaidi ya watu 11,000.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287