Balala azuru bustani ya Mama Ngina kutathmini ujenzi
By Zarina Kassim
Waziri wa utalii Najib Balala amezuru bustani ya Mama Ngina kutathmini ukarabati wa bustani hio unavyoendelea .
Kulingana na waziri Balala, amefurahishwa na jinsi ujenzi unavyoendeshwa huku akisema kuwa ifikapo tarehe 15 mwezi Agousti mwaka huu ujenzi huo utakua umekamilika.
Aidha, Balala amesema kuwa atakua akizuru eneo hilo kila baada ya wiki mbili ili kutathmini ujenzi unavyoendelea. Hata hivyo ameongeza kuwa uunganishaji wa stima umekamilika kwa baadhi ya sehemu.
Kadhalika Balala amewahakikishia wakaazi wa Mombasa na nchi nzima kwa ujumla kuwa hakuna atakaye tozwa ada yoyote ya kiingilio. Akiongezea kwamba biashara zitaimarika na usalama kuimarishwa zaidi katika eneo hilo.