Wanaharakati waandamana Nairobi wakikashifu mashafuko ya Sudan

Maafisa wa polisi wamelazimika kutumia vitoza machozi kulitawanya kundi la wanaharakati waliokuwa wakiandamana katika Bustani ya Uhuru, jijini Nairobi kulalamikia dhulma dhidi ya raia wa Sudan.

Wanaharakati hao wakiongozwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Kutetea Haki za Kibinadam, George Kegoro walikuwa wakiondoka katika bustani hiyo kuelekea bungeni kuwasilisha malalamiko yao wakati walipokabiliwa na polisi na kurushiwa vitoza machozi.

Waandamanaji hao walikuwa wamejumuika na raia wa Sudan wanaoishi humu nchini ambao pia walikuwa wakilalamikia dhulma hizo. Kwa mujibu wa Kegoro, polisi walikuwa wamefahamishwa kuhusu maandamano hao na hata kutoa idhini ila cha kushangaza ni kwamba waligeuka na kuanza kuwakabili.

Hata hivyo inaarifiwa Kamanda wa Polisi katika Kituo cha Central, Simon Kerich alipinga kufanyika kwa maandamano hayo.  Kufikia sasa watu takriban mia moja wameuliwa nchini Sudan tangu jeshi lilipotwaa udhibiti wa nchi kufuatia kujiuzulu kisha kufugwa jela kwa aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Omar Al Bashir.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287