Bunge la kitaifa kujadili tena mgao wa kaunti,Senate imegoma
Bunge la kitaifa linatazamiwa kufanya uamuzi mwingine hapo kesho adhuhuri kuhusu mgao utakaopata serikali za kaunti katika mwaka wa kifedha wa 2018/2019.
Hii ni baada ya Senate kuongezea mapendekezo ya shilingi bilioni 310 yaliyokuwa yamepitishwa awali na bunge la kitaifa hadi shilingi bilioni 335.
Mjadala huo unatarajiwa kuibua hisia kali ikikumbukwa kuwa Maseneta wameapa kuwa hawatokubali kaunti
kupunguziwa mgao illhali serikali ya kitaifa imetangaza uchumi umekua kwa asilimi 6.3.
Wabunge kwenye bunge la kitaifa nao wamesimamia kuwa serikali kwa sasa haina hela na inabidhi kubana matumizi .
Wakati huo huo baraza la magavana nao wameapa kutatua swala hilo mahakamani huku wakiweka bayana hawatofika mbele ya vikao vyovyote vya Senate hadi mzozo huo kutataliwa.
Iwapo bunge la kitaifa litathubutu kupunguza mgao huo itabidi kamati ya pamoja kubuniwa ya maseneta na wabunge la kitaifa kuja na mapendekezo ambayo yatakubaliwa kwenye mabunge yote mawili.
Hii ina maana kuwa serikali za kaunti zitaendelea kusubirishwa kabla kupewa pesa za matumizi ,ingawaje katiba inaruhusu kaunti kupewa kiasi kikubwa cha mgao wao kusimamia huduma muhimu kabla mswada wa kutoa mgao wa kaunti kupita kwenye mabunge mawili.