Museveni aongoza katika kura zinazoendelea kuhesabiwa Uganda

Matokeo ya uchaguzi wa Uganda yanayoendelea kuhesabiwa nchini humo yanadhihirisha kwamba rais Yoweri Museveni angali anaongoza,huku mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Badru Kiggundu akitarajiwa kutangaza matokeo hayo alaasiri ya leo.
Matokeo yaliyotangazwa yanajumuisha kura milioni 7.8 ambazo ni sawa na asilimia 51.2 ya wapiga kura milioni 15 waliosajiliwa na tume ya uchaguzi nchini humo.
Waangalizi wa Umoja wa bara Ulaya pia wanatarajiwa kuhutubia waaandishi wa habari kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda mwendo wa saa sita kasorobo.