Besigje akamatwa kwa mara nyengine

latest02+pix

Wanajeshi wa Uganda wakishirikiana na maafisa wa polisi wamevamia na kuzingira afisi za chama cha upinzani za Forum for Democratic Change (FDC).

Kulingana na ripoti kutoka nchini humo ni kuwa Kizza Besigye amekamatwa katika makao makuu hayo eneo la Najjanankumbi, na wafuasi wa chama hicho wakatawanywa kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi.

 

Hii ni mara ya tatu kwa Besigye kukamatwa wiki hii.

Jana jionio alikamatwa mjini Kampala katika nyumba ambayo upinzani ulidai wizi wa kura ulikuwa ukifanyika.

Siku ya Jumatatu, alizuiliwa kwa muda wakati alipokuwa akifanya kampeni mjini Kampala.