Viongozi wa Pwani wahimizwa kushirikiana

Mwaniaji wa kiti cha useneta kaunti ya Kwale Salim Ali Mwadumbo amewataka viongozi wa pwani kuweka tofauti zao za kisiasa kando na kuja pamoja ili kufanikisha ajenda ya kuwahudumia wakaazi wa pwani kimaendeleo.


Akiongea na wanahabari katika kaunti ya Mombasa Mwadumbo amesema ukanda wa pwani umekuwa nyuma kimaendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi hii ni kutokana na uhasama na tofauti za kisiasa ambazo zimekuwa zikishuhudiwa miongoni mwa wanasiasa hivyo basi kufanya wanasiasa hao kuangazia maslahi yao pasi na kujali shida wanazopitia wakaazi wa pwani.

Aidha Mwadumbo amewasihi vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kama wapiga kura katika zoezi linaloendeshwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ili kuweza kuchagua viongozi ambao watajali maslahi yao na kuwafanyia maendeleo wanayostahili.

 

https://phicmune.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287