IRCK yazindua rasmi ripoti inayoangazia maswala ya jamii na maendeleo Mombasa

Kulingana na ripoti ya kijasusi ya kijamii inayoshughulikia maswala ya kijamii  na maendeleo iliyozinduliwa rasmi katika kaunti ya Mombasa imebainisha kuathirika kwa shughuli za elimu katika maeneo ya likoni kwa kiwango kikubwa.

Kulingana na mwenyekiti wa muungano wa wanawake wa dini mbalimbali Shamsa Abubakar ripoti hiyo imebainisha watoto wengi kutoendelea na masomo wakiwa shule ya msingi,pamoja na uchache wa walimu katika shule mbalimbali umechangia kutatizika kwa shughuli za masomo.

Aidha Shamsa amesema ujio wa corona umefanya wanafunzi wengi wakike kupachikwa mimba na kulazimika kubaki nyumbani.

Shamsa amewataka wahusika wa kila idara kuifanyia kazi ripoti hiyo kuhakikisha wananchi wanafaidika.

Kwa upande wake naibu kaunti kamishna Irene Munyoki amesema ripoti hiyo imeangazia maswala muhimu ambayo serikali inafaa kufatilia ikiwemo maendeleo na usalama.

Irene akisema kulingana na ripoti  ni wazi kuna maafisa wa kiusalama ambao hawawajibiki katika majukumu yao na kuahidi kutafuta njia muafaka ya kusuluhisha hilo.

Vilevile amewataka wanajamii kushirikiana na asasi za kiusalama ili kuhakikisha maafisa wa serikali wanawajibika katika kazi zao.

https://stootsou.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287