wasichana miaka 18 Wachacha Mimba za mapema Kaunti ya Kilifi
Visa hivyo vya dhulma za kijinsia na mimba za mapema zinadaiwa kuongezeaka hasa wakati huu wa janga la korona
Shirika la mawakili wa kike wanaotetea haki za kina mama na watoto FIDA limebaini kuwa asilimia 40 ya wasichana walio chini ya umri wa miaka 18 wamepata ujauzito kaunti ya kilifi.
Mwanasheria katika shirika hilo Amina Abdi anasema wamejitahidi kuhakikisha wanawafikia wasichana wengi kaunti hiyo kuwaelimisha dhidi ya kujiepusha na janga la mimba za utotoni.
Amina amesema kuwa maafi kutoka kwa shirika hilo wako nyanjani ili kukusanya maoni jinsi wanavyonyanyashwa sawia na changamoto wanazopata.
Wakati huo huo Amina ameweka wazi kwamba sababu zinazochangia mimba za utotoni katika jamii ni umaskini, hali anayosema kuwa imewalazimu kufadhili baadhi ya makundi ya kinamama ili wajiendeleze kibiashara lengo likiwa nikukabili umaskini katika jamii.