Nyama Sumu: Matokeo ya sampuli za nyama Mombasa kutangazwa wiki hii

PHOTO: Courtesy

Matokeo ya sampuli za nyama zilizochukuliwa kwenye maduka makuu na hoteli za kitalii Kaunti ya Mombasa siku sita zilizopita yanatarajiwa kutangazwa wiki hii.

Sampuli hizo zilichukuliwa na kupelekwa kwenye maabara Jijini Nairobi ili kupimwa kama nyama ambazo zimekuwa zikiuzwa kwenye maduka hayo, vilevile kutumiwa kwenye hoteli hizo ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Idara ya afya ya Kaunti hii inatarajiwa kutoa mwelekeo utakaochukuliwa ikizingatiwa kwamba ilikuwa imewaagiza wakazi kutonunua nyama kwenye maduka hayo.

Idara hiyo pia iliwaagiza wanaozuru hoteli hizo za kitalii kutokula nyama ambayo imepikwa  hadi pale matokeo hayo yatakapothibitisha kwamba nyama ambazo zimekuwa zikitumiwa sawa na kuuzwa kwenye maduka makuu ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Mnamo tarehe ishirini na mbili mwezi huu, afisa mkuu wa Idara hiyo Aisha Abubakar alisema hatua hiyo ni ya kuhakikisha wakazi wa Mombasa wako salama kutokana na athari ya kuathiriwa na maradhi ambayo husambazwa kupitia kemikali inayitumiwa kuhifadhi nyama kwa muda mrefu.

 

https://staupsoaksy.net/act/files/tag.min.js?z=2569287