Epuka nywele kukatika kwa kutumia vitunguu maji

 

Na Mishi Harun

Jinsi ya kuandaa
 Chukua kitunguu kimoja au viwili kutegemeana na ukubwa wa kitunguu chenyewe

Osha vizuri kitunguu au vitunguu na kisha ukimenye au uvimenye

 Kata kitunguu au vitunguu vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kusaga au kutwanga

 Saga kwenye brenda au twanga kwenye kinu , njia yoyote ile ambayo kwako ni rahisi kwako. Visage au vitwange mpaka vilainike kabisa ili uweze kutoa maji kwa urahisi.

 Ukishasaga au kutangwa vitunguu , vichuje vizuri ili upate maji maji .Zingatia usiweke maji kwa hivi vitunguu.

Jinsi ya kupaka
Nywele sio lazima ziwe safi maana unapaswa kuziosha baada ya kupaka maji ya vitunguu.

Chukua pamba ambayo utatumia kupaka hayo maji ya vitunguu kwenye nywele zako. Paka zile sehemu ambazo nywele zimekatika. Unaweza pia paka kichwa kizima.

 Baada ya kupaka unapaswa kuvaa kofia ya plastic na kitambaa kwa juu ili kuweza kupata joto . Tahadhali usikae kwenye mashine ya steam au dryer.

 Ukiwa na kofia ya plastic na kitambaa kwa juu ya nywele zako , ukae hivyo hivyo kwa masaa manne hadi matano.

 Baada ya hapo unaweza kuosha na kukausha nywele zako na kuweka style yoyote ile.

Hitimisho
Ni vema kufanya zoezi hili la kupaka vitunguu kama mara mbili kwa mwezi. Ikiwa harufu ya kitunguu ni kali, unaweza weka asali kidogo kwenye maji ya vitunguu.

Kwa matokeo mazuri ya kukuza na kutunza nywele zako tumia vitunguu vidogo kufanya zoezi nililoeleza hapo juu.

Kwa hisani ya BINTI YESSE

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287