Wazalishaji wa bidhaa za mafuta waiomba serikali kuwapunguzia ushuru
Wazalishaji wa bidhaa za mafuta nchini wameendelea kuishinikiza serikali dhidi ya kuiinglia kati ushuru unaotozwa kwa wafanyibiashara wa humu nchini ,wanaposafirisha bidhaa zao katika masoko ya afrika masharaki.
Rajul Malde ambaye ni mkurugenzi wa biashara katika kampuni ya uzalishaji wa bidhaa za mafuta na sabuni nchini ya Pwani Oli,anasema wao hukatwa asilimia 10 wanaposafirisha bidhaa zao kuelekea Uganda, huku wafanyibiashara wa Uganda na Afrika Mashariki, wakiuza bidhaa zao humu nchini kwa viwango vya chini.
Malde anasema kuwa wamekuwa wakisafirisha zaidi ya trela nne za bidhaa zao lakini kutokana na ushuru huo wanasafirisha trela mbili pekee,jambo linalozorotesha biashara zao katika ushindani wa Afrika Masharaki.
‘’Tumekuwa tukituma tukituma matrela manne ya bidhaa zetu katika taifa jirani la Uganda,wakati tukianza,mwezi wa Jannuary,February na Machi,lakini kuanzia mwezi wa Aprili baada ya kuanzishwa kwa ushuru wa asilimia 10 kwa taifa la Uganda,Tumeanza kusafirisha matrela mawili pekee.’’Alisema Malde.
“Kwa trela moja huwa lenye bidhaa hugharibu dola elfu 35,hii inamaana tulipokuwa tukisafirisha matrela manne ya bidhaa ilikuwa na gharama ya dola elfu 140.”Aliongeza Malde.
Aidha Malde anasema wamekuwa wakikatwa ushuru wa asilimia 2 nchini wanapoagiza bidhaa ghafi kutoa mataifa ya nje ,ila mataifa yaliyoko katika afrika mashariki hayakatwi lolote.
Hatahivyo ameipongeza serikali ya Kenya kwa kuanngazia masuala ya usafirishaji wa bidhaa za wafanyibiashara ,kama ilivyotajwa na waziri Henry Rotich kwenye bajeti.
Ikimbukwe katika bajeti ya mwaka huu 2019/2020 ,sekta ya uzalishaji viwanda ambayo ni moja wapo ya Jenda 4 kuu za serikali ya jubilee,imetengewa shilingi billion 1.1 kukuza sekta hiyo.
Kampuni ya Pwani Oil ambayo iliasisiswa mwaka 1981, ni mojawapo ya kampuni kubwa nchini,inayosafirisha na kusambaza bidhaa zake nchini na mataifa afrika mashariki,ikiwemo Tanzania,Uganda na Rwanda.