BAADA YA DHIKI HATIMAYE FARAJA
Takriba siku tatu baada ya Riak Machar kuapishwa kama makamu wa Rais nchini Sudan Kusini, viongozi hao wakiwemo mawaziri wapya wa serikali hiyo ya muungano wamejitokeza nje na kupiga pichakwa pamoja kama ishara ya kuonyesha kurudi kwa amanai katika taifa hilo.
Sudan kusini imekuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka miwili baada ya Rais wa taifa hilo Salva Kiir kumuachisha kazi Riek Machar kama makamu wake kwa madai ya kutaka kupindua serikali yake.
Viongozi hao walikubali kutekeleza mkata wa amani uliotiwa sahihi hapo awali baada ya shinikizo kutoka kwa mataifa ya magharibi.
Machar aliapishwa tena kama makamu wa Rais mnamo siku ya Jumanne wiki hii hatua ambayo inashuhudiwa kuwa muhimi katika kuregesha amani nchini humo.
Viongozi mbali mbali wamepongeza hatua hiyo na kuwataka viongozi hao kushirikiana kwa minajili ya kuboresha usalama, kudumisha amani na uimarishaji wa uchumi wa taifa hilo.