RAIS WA AFRIKA KUSINI MASHAKANI KWA TUHMA ZA UFISADI.
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma
Huenda Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma akajikuta mashakani baada ya mahakama kuu nchini humo kutoa uamuzi kuwa kesi 783 za ufisadi dhidi yake zinafaa kuregelewa upya.
Kesi hizo zilitupiliwa mbali wiki chache tu kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2009 ambapo Zuma alichaguliwa kama Rais wa taifa hilo.
Jaji wa mahaka hiyo Audbrey Ledwaba amesema kuwa kiongozi wa mashtaka katika upande wa serikali alitoa uamuzi huo bila kuzingatia katiba wa taifa hilo.
Zuma amekuwa akikanusha madai ya ufisadi ambayo yamekuwa yakimhusisha pamoja na serikali ambapo mabilioni ya pesa yanadaiwa kupotea.
Kesi hiyo iliyowasilishwa na chama cha upinzani cha Democratic Alliance inawapa viongozi wa mashtaka nafasi ya kuregesha tena kesi hizo mahakamani.
Mahakama hiyo inasema kuwa uchunguzi upya wa simu inaonyesha kuwa kesi hizo ziliingiwa na kisiasa na hivyo basi ipo haja kuregelewa tena.
Hata hivyo chama tawala cha ANC kimepinga hatua hiyo kikisema kuwa mahakama haikumpata Rais huyo na kosa lolote.
Mapema mwezi jana, Rais Jacob Zuma aliponea chupuchupu baada ya wabunge kutoka upinzani kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani naye kwa sababu ya kuhusika katika visa vingi vya ufisadi.