Waathiriwa wa mashambulio ya viboko Kilifi wataka kufidiwa

Waathiriwa Mashambulio ya Viboko katika kijiji cha Moye karibu na mto Sabaki  kaunti ya Kilifi sasa  wanaitaka serikali  kuwafidia  kutokana na athari walizozipata kufuatia uvamizi wa mara kwa mara wa viboko katika mashamba yao.

Waathiriwa hao wakiongozwa na Changawa mwajombo wanasema kuwa licha ya wao kuwasilisha maombi  ya kupata fidia kwa shirika la huduma za wanayapori nchini KWS bado maombi hayo  hayajashughulikiwa huku familia zao zikiendelea kutaabika .

Aidha Wakaazi hao  wameelezea hofu yao kufuatia  mashambulizi ya wanyama hao yanayozidi kuongezeka kila siku  huku wakiitaka serikali kupitia shirika ka KWS   kuchukua hatua ya haraka  na kuweka ua katika eneo hilo  ili kudhibiti maafa zaidi  yanayosababishwa na wanayama hao.

 

https://jouteetu.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287