Vijana Mombasa wahimizwa kuendelea kudumisha amani
Wito umetolewa Kwa vijana Kaunti ya Mombasa kuendelea kudumisha amani na uwiano hata baada ya kukamilika kipindi cha uchaguzi mkuu Nchini.
Akiongea katika uga wa Bofu wakati wa michuano ya kandanda inayonuia kuweka uwiano baina ya vijana kwenye Kaunti hiyo, Mwenyekiti wa Shirika la Mombasa Women of faith Shamsa Abubakar maarufu Mama Shamsa amewapongeza vijana wa Kaunti hiyo Kwa kudumisha amani katika uchaguzi mkuu uliyopita, licha ya kuwa ilikuwa imeoridheshwa na tume ya NCIC kuwa miongoni mwa Kaunti zilizokuwa katika hatari ya kuzuka ghasia za Uchaguzi.
Aidha amewarai vijana kwenye Kaunti hiyo kutumia michezo ili kuwaunganisha pamoja na kuwavutia wenzao kujiunga na Mashirika ya uenezaji wa amani.
kauli yake imeungwa Mkono na naibu Kaunti kamishna wa eneo la changamwe Tom Konyele ambaye amewatahadharisha vijana dhidi ya kuchochewa na watu wenye maslahi binafsi kuzua ghasia, akiwahimiza kudumisha amani Kwa ajili ya kuendeleza jamii.
Kwa upande Mariana Akinyi kutoka Baraza la uwiano wa dini mbalimbali IRCK amedokeza kuwa wanatekeleza miradi kadhaa katika inayolenga kuwahamasisha vijana kudumisha amani,akiwahimiza kushiriki miradi hiyo Kwa ajili ya kujiendeleza.
Naye mwakilishi kutoka Shirika la Mombasa Interfaith youth Network Omar Chai, amewarai vijana wanaojihusisha na magenge ya wahalifu Kaunti ya Mombasa kujisalimisha katika taasisi husika za serikali ili waweze kujinasua ,akisema kuwa kuwa jamii iko tayari kuwapokea endapo wataamua watabadili mienendo yao.