Viongozi wa Dini ya Kiislamu katika kaunti ya Mombasa waitaka serikali kuelezea alipo Profesa Hassan Nandwa

Viongozi wa dini ya kiislamu katika kaunti ya Mombasa wameitaka serikali kuelezea alipo mhadhiri na wakili  Profesa Hassan Nandwa.Hii ni baada ya wakili huyo kutoeka katika mazingira ya kutatanisha.

Wakiongozwa na Imam wa msikiti wa spaki katika kaunti ya Mombasa Sheikh Abu Hamza,amesema Nadwa amepotea baada watu wanaodaiwa kuwa maafisa wa polisi kuvamia nyumbani kwake Nairobi maeneo ya Ngong na kumkamata.

 

 

Abu Hamza akisistiza kuwa iwapo muhadhiri huyo amefanya makosa ya kisheria  basi afikishwe mahakamani na haki ifate mkondo wake.

 

 

Aidha Abu Hamza amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati kuongea na taasisi za kiusalama kuhakikisha mhadhiri Nandwa anapatikana.

Vile vile Viongozi hao wamekemea kuongezeka kwa visa vya kupotezwa kwa waislamu bila kupatikana.

 

 

Kauli za viongozi hao zinajiri baada ya vyama vya kutetea maslahi ya waislamu,vyama vya kutetea haki za kibinadamu na chama cha mawakili nchini LSK kutaka serikali  kuelezea alipo wakili Nandwa

https://upskittyan.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287