Hofu ya kunyanyaswa kimapenzi ndani ya karantini, KMTC Mombasa
photo credit; google
Wanafunzi 17 waliokuwa wamewekwa karantini katika kituo cha taasisi ya Mafunzo Utabibu KMTC hapa Mombasa tangu kurejea nchini kutoka Sudan wameruhusiwa kujiweka karantini wakiwa nyumbani.
Hatua hiyo inajiri baada ya baadhi ya wanafunzi hao wakike ambao walikuwa wanahofia kunyanyaswa kimapenzi na baadhi ya wanaume ambao wamewekwa karantini katika kituo hicho.
Hata hivyo wanafunzi hao wamepewa maelekezo na idara ya afya ya kaunti ya Mombasa ya jinsi kujiweka karantini wakiwa nyumbani ili kuzuia uwezekanao wa maambukizi zaizi.
Ikumbukwe jana wazazi wa wanafuzi hao walielezea kusikitishwa kwao kufuatia malalamishi kutoka kwa wanafunzi bila ya hatua kutochukuliwa.