Makali ya Virusi Vya korona yaangamiza Raia 12 Nchini, Nairobi ikiongoza kwa maambukizi

 

Makali ya virusi vya Korona yanazidi kushuhudiwa nchini baada ya watu 12 zaidi kuaga dunia na kufuikisha idadi jumla ya waliofariki hadi 250.

Watu 397 hii leo wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo na kuongeza idadi ya maambukizi hadi 14,168 kote nchini.

Katibu katika wizara ya Afya Dk. Rashid Aman amesema takwimu hizo zimetokana na vipimo vya sampuli 3,637zilizopimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Aidha Rashid amesema kuwa miongoni mwa kesi zilizothibitishwa hii leo watu 389 ni wakenya huku wanane wakiwa ni raia wakigeni.

Kaunti ya  Nairobi inaendelea kuandikisha idadi ya juu ya maambukizi ya Korona 239 huku serikali ikiendelea kuwahimiza wananchi kuzingatia sheria zilizowekwa kwani imebainika kuwa wazee ndio wako kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa virusi hivyo kutokana na umri wao mkuu.

Vile vile Kaunti Kiambu imeripoti visa 33, Machakos 27, Nyeri 17, Busia 16, Nakuru 12, Mombasa 12, Kajiado 10, Migori 8, Uasin Gishu 8, Kericho 5, Narok 3, Laikipia 3 na kaunti ya  Kisii, Nyandarua, Kisumu pamoja Lamu vikipata 1 kila mmoja.

Hata hivyo  watu 642 wamethibitishwa kupona na kufikisha idadi jumla ya waliopona kuwa 6,258.

mwandishi; Geoffrey Chiro.
https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287