‘Tumechoshwa na mabwenyenye wanyakuzi wa ardhi’, Ghadhabu za wakaazi Jomvu kuu
photo courtesy;
Wakaazi wa eneo la Jomvu Kuu kaunti ya Mombasa wameelezea kughadhabishwa kwao na hatua ya baadhi ya mabwenyenye waliojitokeza na kutaka kunyakua ardhi yao.
Kulingana na mzee wa mtaa wa eneo hilo Salim Widad Salim, Mabwenyenye hao walikaribishwa na wakaazi wa eneo hilo na kupewa ardhi miaka ya nyuma na hivi sasa wanadai kuwa wamiliki wa ardhi hizo hali inayolazimisha zaidi ya familia elfu kumi za wenyeji hao kuenda kutafuta makaazi kwengine.
Ameongeza kuwa licha ya kuwasilisha malalamishi yao kwa Kamishna wa Kaunti pamoja na Seneta wa kaunti ya Mombasa Mohamed Faki, bado kilio chao hakijasikizwa
mwandishi ; Geoffrey Chiro