Zaidi ya wafanyikazi 300 wa Leopard Beach Resort kutolipwa marupurupu kwa zaidi ya miaka 2
Kufuatia kuchomeka kwa Hoteli ya Leopard eneo la Diani kaunti ya Kwale miaka miwili iliyopita na sasa wafanyikazi wanaitaka serikali kuingilia kati na kuhakikisha kuwa wanapata haki yao.
wafanyikazi hao wasiopungua 300 katika hoteli hio wanalalamikia kutolipwa malimbikizi ya marupurupu yao wanayodai hoteli hiyo kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
Wafanyikazi hao wanaidai hoteli hiyo zaidi ya shilingi milioni 41 na wanasema kuwa kwa sasa wanapitia hali ngumu ya maisha hasa baada ya janga la korona kuingia nchini.
Hata hivyo Kwa upande wake msimamizi wa hoteli hiyo Kioko Munyoki ametetea hoteli na kusema kuwa kutolipwa kwa wafanyikazi hao kunatokana na mkasa huo wa moto.