Zaidi ya bilioni moja yatengewa wakaazi wa eneo la Owino Uhuru
By Salma Mohammed
Mahakama ya mazingira humu nchini imeamuru serikali kulipa fidia ya shilingi bilioni 1.3 kwa wakaazi wa eneo la Owino Uhuru, changamwe walioathirika na sumu aina ya Lead iliyokuwa ikitoka kwenye kiwanda kimoja eneo hilo.
Kesi hiyo iliyowasilishwa na wakaazi wa eneo hilo pamoja na wanaharakati mbalimbali mwaka 2016, ilinuia kudai fidia kwa ajili ya wapendwa wao waliopoteza maisha na wengine kupata maradhi ya kiafya kutokana na sumu hiyo.
Aidha wameeleza kufurahishwa kwao na uamuzi wa mahakama licha ya kuwa kesi ilichukuwa muda mrefu kukamilika.