Kenya kupokea madakatri kutoka Cuba kusaidia sekta ya afya

By Fatma Rajab

Kenya leo hii itapokea madaktari 20 kutoka nchi ya Cuba ambao watasaidia katika utafiti wa kukabiliana na maradhi mbali mbali nchini ikiwemo covid-19.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema madaktari hao wataingia nchini leo usiku na watahudumu katika chuo cha kimatibabu cha Kenyatta.

Amesema madaktari hao watahudumu humu nchini kwa miezi 6.

Kagwe ameongeza kuwa  kutokana na kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya virusi vya korona nchini, madaktari hao watasaidiana pakubwa na madaktari wa humu nchini katika vita dhidi ya virusi hivyo.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287