serikali yaombwa kuwahusisha walemavu kwenye miradi wanayoitoa ikiwemo kazi mtaani.
by jeff chiro
Mwenyekiti wa shirika la jamii la watu wanaoishi na ulemavu la Step 001 hapa Mombasa Salim Mwachupa Mazera ameiomba serikali kuwatambua walemavu kwenye miradi mbali mbali inayotolewa na serikali ikiwemo kazi mtaani.
Salim amesema inasikitisha kuona kwamba serikali imetoa mradi wa kazi kwa vijana lakini kwenye mradi huo jamii ya walemavu hawahusishwi.
Aidha amesema kuwa jamii ya walemavu wamekuwa wakibaguliwa serikali huku akitoa wito kwa serikali kuwa wanahaki kama mwananchi mwengine wa kawaida.
Salim aidha ametoa wito kwa serikali kuu kushughulikia masuala ya watu wanaoishi na ulemavu akisema jamii zote zinafaa kushirikishwa kwenye miradi mbali mbali ya serikali.
Zaidi amesema tangu kuibuka kwa janga la virusi vya corona walemavu wengi pia wamekuwa bila kazi ikizingatiwa kuwa baadhi yao wanakumbwa na majukumu ya kifamilia.