Zaidi ya vijana elfu 3 kunufaika na mradi wa kazi mtaani kaunti ya Kwale.
By popoo
Zaidi ya vijana elfu 3 kutoka sehemu mbali mbali kaunti ya Kwale watanufaika na mradi wa kazi mtaani.
Kulingana na kamishna wa kaunti hiyo Karungu Ngumo, awamu ya pili ya mradi huo itatekelezwa kwa zamu ya baada ya wiki mbili.
Hata hivyo ameweka wazi kuwa malipo ya vijana hao yamepunguzwa kuwawezesha vijana wengi kunufaika na mpango huo.