Mvua kubwa yatarajiwa kunyesha hivi leo hadi siku ya Jumalipi.

Na Francis Mwaro

Mvua kubwa ambayo ilishuhudiwa wiki iliyopita katika sehemu mbali mbali nchini  inatarajiwa kunyeshesha tena kuanzia hivi leo.

Mvua hiyo inatarajiwa kunyesha kwa kiwango cha zaidi ya milimita 20 kwa muda wa masaa ishirini na nne inatarajiwa kunyesha hadi siku ya Jumapili mfululizo.

Katika sehemu ambazo zinatarajiwa mvua hiyo ni ikiwemo ,Nairobi ,kusini mwa kati na maeneo mwa kati mwa nchi .

Kaunti za Mombasa ,Kwale ,Kilifi ,Tana River na Lamu pia zinatarajiwa kushuhudia  mvua kubwa .

Wakazi ambao wanaishi maeneo hayo wametahadharishwa na kuwa makini wakihimizwa kutoendesha magari na kutembea katika maji ambayo yanatembe kwa kazi kulingana na idara ya utabiri wa hali ya anga nchini.

Siku mbili zilizopita mvua ambayo ilishuhudiwa katika eneo la Mombasa ilisababisha uharibifu mkubwa kwa wakazi pamoja  na barabara kururika maji.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287