Aisha Jumwa azuilwa katika kituo cha polisi cha Kilindini.
Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa ametiwa mbaroni jana usiku kwa kuhusishwa na vurugu ambazo zilisababisha mtu mmoja kupigwa risasi na kuuwawa katika wadi ya Ganda.
Mbunge huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilindini akisubiri kupelekwa mahakama na kufunguliwa mashtaka.
Hata hivyo Jumwa amejitenga na vurugu hizo akitaka idara husika za usalala kufanya uchunguzi wao na kuwatia mbaroni wahusika wote ambao walisababisha vurugu hizo .
Jumwa vile vile amesema alikuwa alienda kuulizia ni kwa njia gani kuliandaliwa mkutano katika boma ya mgombea wa chamba cha ODm Rueben Katana kinyume na sheria baada ya siku za kufanya kampeni zikiwa zimeisha.
Vurugu hizo zilitoke pale wafuasi wa chama cha ODM walioanza kumrushia mbunge huyo wakati maafisa wa polisi walikuwa katika eneo hilo kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya umati huo.
Haijabainika ni nani aliyeweza kufyatua risasi hiyo na kumuua jamaa huyo ambaye ni mmoja wa familia ya mwaniaji wa kiti hicho kupita chama cha ODM.
Seneta mteule kaunti ya Kilifi Cristine Zawadi ni miongoni mwa viongozi ambao walifika katika kituo cha polisa cha Kilindi huku wakili wake Jerald Magolo akiwa bado hajaruhusiwa kumuona mteja wake.
Uchaguzi huo mdogo utafanyika hapo kesho baada ya tume ya uchuguzi na mipaka IEBC kufatilia mbali uchaguzi huo wadi ya Ganda.